Top Stories

Askari Koplo Yusuph ajinyongwa kwenye nyumba aliyoijenga (+video)

on

Askari wa Jeshi la Polisi aliyekuwa anafanya kazi katika kituo cha Polisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani  namba E 6472  Yusuph Said (52), amekutwa  amejinyonga hadi kufariki dunia  katika  nyumba yake anayoijenga maeno ya miembe saba  Kata ya Kongowe Wilayani Kibaha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, amethibitisha  kutokea kwa tukio hilo Januari 18 majira ya saa 12 jioni.

Kamanda Wankyo amesema Yusuph alikua akitumikia katika kituo C anaishi Picha ya ndege lakini siku ya tukio alienda Kongowe eneo ambalo anaendelea na ujenzi na ndipo alipokutwa amejinyonga na kamba.

Kamanda Nyigesa, amebainisha kuwa, uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea wakati taratibu za kumsafirisha marehemu kuelekea mkoani Lindi kwa maziko zikiendelea.

 

Soma na hizi

Tupia Comments