Waziri wa Nishati, January Makamba ametembelea mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere Agosti 08 2022 ili kukagua na kuangalia hatua mbalimbali zilizofikiwa na mradi huo.
Mara baada ya kukagua mradi huo Waziri Makamba amesema >>‘ Mradi huu umeanza kujengwa Disemba 2018 kwa sasa tumefika asilimia 67, Katika Miaka Miwili na nusu ya Mwanzo (Kuanzia Disemba 2018 – June 2021) tulifikia asilimia 37. Leo tuko asilimia 67 ni kasi kubwa katika kipindi hiki kifupi, Sasa hivi hapa kazi inafanyika saa 24 hakuna mapumziko kwa hiyo kasi imeongezeka‘ – Waziri Makamba.
Waziri Makamba kwenye ziara yake kwenye Bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere amembatana na Bodi ya Wakurugenzi Tanesco, Menejimenti ya Tanesco ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Ndg. Maharage Chande na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari.