Top Stories

Askofu avuliwa cheo kisa uzinzi

on

Kanisa la Anglican Nchini Uganda limemvua cheo aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Stanley Ntagali, na kusitisha utendaji wa majukumu ya Uaskofu pamoja na kuzuiwa kuwakilisha Kanisa hilo kutokana na madai ya uzinzi.

Ntagali alistaafu mwaka jana Machi baada ya kuhudumu kwa miaka 43 kama Askofu na anatuhumiwa kujihusisha kimapenzi na Mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye ndoa huku askofu huyo alilifahamu hilo.

Taarifa ya Kanisa imesema, Ntagali alisaliti Ofisi ya Askofu, kiapo alichokula wakati wa kuapishwa na maadili mema aliyotekeleza kwa kujitolea. Kanisa la Anglican Nchini Uganda linakadiriwa kuwa na wafuasi Milioni 13.

MSAKO USIKU WA MANANE, SABAYA AVAMIA GODOWN HEWA AKUTA MAGENDO, PESA, MAFUTA NA POMBE

Soma na hizi

Tupia Comments