Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima amekataa kuketi katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na badala yake alitaka kusimama muda wote wa kikao hicho cha kamati.
Askofu Gwajima aliitwa kuhojiwa kwa mara ya kwanza katika kamati hiyo Agosti 23, 2021 ambapo anatuhumiwa kwa kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.
Sasa leo Agosti 25, 2021 ni mara ya pili kufika katika kamati hiyo baada ya mara kwanza shauri hilo kutomalizika.
Mara ya kwanza Askofu Gwajima alitaka kubadilishiwa kiti na kipaza sauti jambo ambalo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka alilikubali na kuagiza kubadilishwa kwa kiti na kipaza sauti kama alivyoombwa.
ASKOFU AMALIZA KUHOJIWA ASEMA “WAKISEMA NA MIMI NITASEMA”