Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima alifika katika viwanja vya bunge majira saa 6:35 kuitikia wito uliomtaka kufika mbele ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge.
Askofu Gwajima alikaa Takribani saa 1 na nusu akisubiri kuitwa na Kamati na muda ulipofika alitakiwa kuingia kwenye ukumbi ambao kamati walikuwa wakimsubiri lakini taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa Kamati, Emmanuel Mwakasaka alisema shahidi ambaye ni Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima kuna dawa anaitumia tuendelee kumsubiri amemuagiza dereva.
“Sina taarifa ya shahidi kama ana tatizo lolote la kiafya linalomtaka shahidi ameze dawa kwanza ndio aje kwa hiyo tuendelee kumsubiri inawezekana limempata baada ya kufika hapa”
Muda mchache baadae Askofu Gwajima aliingia katika ukumbi waliokuwepo kamati na akaomba kubadilishiwa kiti kilichokuwa kimeandaliwa kwa ajili yake na kubadilishiwa kipaza sauti (Mic) kilichokuwa kimeandaliwa kutumia yeye kuongelea hali iliyokubaliwa na wajumbe wa kamati hiyo na baada ya muda mhudumu wa Bunge alibadilisha vifaa hivyo na kamati kuanza kumuhoji.
ASKOFU GWAJIMA ALIVYOTINGA BUNGENI DODOMA KUHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI