AyoTV

Aslay kaongea kwanini hayuko tena na Mwanamke aliyekua na ujauzito wake… Umeneja mpya je?

on

Aslay ni mwimbaji kutokea kundi la Yamoto BAND, kilichofanya awepo kwenye hii post ni kauli yake ya kukanusha kumtelekeza Mwanamke mwenye ujauzito wake baada ya kuishi nae kwa miezi isiyozidi 6.

Aslay ambaye ana umri wa miaka 20 sasa hivi amesema ‘Baada ya kuishi pamoja miezi sita tulizinguana ikabidi kila mtu ashike hamsini zake, sisi vijana bwana mambo mengi… tukaangalia pia mimi bado umri wa kukaa na Mwanamke na yeye akaona bado umri wake wa kukaa na Mwanaume

aslay 3

Aslay na mzazi mwenzie

Sikuchukua uamuzi ila wote ndio tulichukua uamuzi…. nilimuacha na ujauzito wangu na tayari amejifungua mtoto wa kike ambaye ana kama mwezi mmoja na nusu, mwanangu nimemuita Moza jina la marehemu mama yangu… na bado mpaka sasa tunaonana hata hapa nimetoka kumuona mwanangu, hatujarudiana…. tunashirikiana tu kama mtu na mzazi mwenzake‘ – Aslay

Kingine alichokiongea Aslay kwa sasa ni kwamba amekabidhiwa majukumu mapya ya kuwa meneja, aliyemkabidhi ni boss wake Mkubwa Fela kiongozi wa Mkubwa na Wanawe na sasa Aslay ni meneja wa madada watano aliokabidhiwa miezi mitatu iliyopita na watasikika very soon.

Unaweza kumtazama Aslay hapa chini..

UNAPENDA BONGO MOVIE? TAZAMA HIKI KIPISI CHA MATRON ALIYEMPENDA MWANAFUNZI MTUKUTU.. NISHA KAONYESHA UWEZO HUMO NDANI…

https://www.youtube.com/watch?v=bFp4y3bgu0U

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments