Habari za Mastaa

Hamisa Mobetto ameanza kuimba? hiki hapa kionjo cha wimbo wake

on

Model Hamisa Mobeto ametengeneza wimbo mpya alioupa jina la Madam Hero ambao ni moja ya wimbo wake mpya kwa ajili ya Foundation yake inayofahamika kama The Mobetto Foundation ukiwa na ujumbe wa kuhamasisha wanawake kutokata tamaa na kusonga mbele.

Hamisa Mobetto ambaye amesema kuwa wimbo huo atauachia soon kwenye moja ya Apps za Muziki na kila pesa itakayokuwa ikipatikana atakuwa aikiipeleka kwa Wanawake wanaolea watoto katika maisha magumu au wanawake wanaojifungua katika hali ngumu.

Kupitia Instagram Hamisa ameweka sehemu ya wimbo huo na kuambatanisha na Caption iliyosomeka…..…….>>>>”I have been through a lot kusema kweli 🙌🏽!!! …. lakin pia sina wa Kumlaumu wala haja ya kulalamika kwasababu kila mtu ana opinion yake kwenye situation yangu na hakuna anaeujua ukweli zaid ya mie Muhusika mwenyewe……

“But naamini katika kuipa tabasamu , jamii inayonizunguka , wamama wanaonizunguka na wadada wanaonizunguka !! Sikupanga Njia yangu iwee hii but Naona mwenyezi Mungu anasababu zake !!! I hope mtaupokea wimbo wangu huu wa Madam Hero ambao ni moja ya Nyimbo za Kwenye Foundition yangu ya @themobettofoundation kama Nguvu ya kupambana , kutokukata tamaa na kuangalia mbele kwa kila mwanamke aliyechaguliwa kupitia barabara kama yangu 😰🙏🏾”

“Nyimbo hii nlirecord mwaka jana kwenye studio ya @c9kanjenje @c9records
Chini ya Tizi na Usimamizi wa @fobyofficial ….. Soon nitaachia kwenye moja ya Apps ya Muziki na kila pesa itakayopatikana kutoka kwenye manunuzi ya Nyimbo hii a Madam Hero itawaendea Wamama wanaolea watoto katika maisha magumu Au wanaujifungua Katika Hali Ngumu… In shaa Allah 🙏🏾 #MadamHero ….. soon In God We Trust ❤️✅” – Hamisa Mobetto

MC Pilipili amezungumzia aliyefungua Shampein kwa mdomo “nilimwambia fungua kwa mdomo”

Kitakacho kushangaza, Staa wa zamani Man City kwenda kula Uswahilini Mwananyamala

Soma na hizi

Tupia Comments