Michezo

VIDEO: Liverpool wamefunga mwaka kwa kuiadhibu Man City ya Pep Guardiola

on

Baada ya shauku na presha za mashabiki wa soka waliyokuwa wanasubiria kwa hamu mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Englnd kwa mwaka 2016 kuchezwa, usiku wa December 31 mchezo huo uliyokuwa unazikutanisha timu za Liverpool aliyekuwa nyumbani dhidi ya Man City ndio ulichezwa.

3bbcebf900000578-4078642-image-a-36_1483211131345

Liverpool wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Anfield na kocha wao Jurgen Klopp walifanikiwa kuiadhibu Man City ya Pep Guardiola goli 1-0, goli ambalo lilifungwa dakika ya 8 na Georginio Wijnaldum aliyetumia vyema assist ya Lallana na kuifanya Man City kupoteza mchezo wa nne wa EPL msimu wa 2016/2017.

screen-shot-2016-12-31-at-11-14-34-pm

Msimamo wa EPL baada ya mechi 7 kuchezwa Jumamosi ya December 31 2016.

Kwa matokeo hayo Man City wanakuwa wamepoteza jumla ya michezo 101 kati ya michezo 205 waliyowahi kucheza dhidi ya Liverpool huku wakiwa wameambulia sare mara 53, mara ya mwisho Liverpool kupoteza dhidi ya Man City katika mchezo wa EPL ilikuwa August 25 2014 kwa goli 3-1 katika uwanja wa Etihad.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments