Michezo

Aston Villa waishukuru Tanzania kwa mapenzi yao kwa Samatta

on

Mtanzania Mbwana Samatta jana kwa mara ya kwanza aliichezea Aston Villa katika mchezo wa nusu fainali ya Carabao Cup dhidi ya Leicester City, mchezo huo ambao Samatta alicheza kwa dakika 66, Aston Villa walitinga fainali kwa ushindi wa magoli 2-1 (agg 3-2).

Kwa upande wa Tanzania mashabiki sehemu mbalimbali walijumuika kwa pamoja na kuangalia mchezo huo wa kihistoria kwa nchi, huku kwao Mbagala kulikuwa na LIVE Big Screen, mashabiki lukuki wakiongozwa na baba mzazi wa mchezaji huyo mzee Pazi walikuwa pamoja na leo twitter account ya Aston Villa wamepost video hiyo kuwashukuru watanzania kwa sapoti.

VIDEO: RAHA ILIYOJE !!! BABA MZAZI WA SAMATTA, HAKULALA ANACHEZA MUZIKU UTAMBULISHO WA ASTON VILLA

Soma na hizi

Tupia Comments