Club ya Aston Villa imetangaza rasmi kumsajili nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta akitokea KRC Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne na nusu.
Samatta yupo Villa Park hadi (2024) kocha wa Aston Villa Dean Smith mapema leo akiongea na waandishi wa habari alisisitiza kuwa mchezaji huyo kila kitu kimekamilika bado vitu vidogo tu.
Hata hivyo Samatta ,27, hatoweza kucheza mchezo wa kesho wa Aston Villa dhidi ya Watford kwa kuwa hakupata muda wa kutosha kuwa na timu hiyo kutokana na kuchelewa kupata kibali cha kazi.