Ikiwa leo ni siku ya tatu mfululizo washtakiwa wanne wanaokabiliwa na kesi ya ubakaji kwa kundi na ulawiti wamefikishwa tena katika Kituo cha Utoaji Haki, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma.
Katika kesi hiyo nambari 23476 ya mwaka 2024, washtakiwa hao wanadaiwa kumbaka kqa kundi na kumlawiti binti aliyejitambulisha anatokea Yombo Dar es Salaam.
Washtakiwa hao ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo,Amin Lord Lema ,Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi wamefikishwa na gari la Jeshi la Magereza wakiwa na watuhumiwa wa kesi nyingine zinazoendelea mahakamani hapo.