Michezo

Ujumbe alioandika dogo wa miaka sita kumuomba Mourinho aiokoe Aston Villa…

on

Shabiki mwenye umri wa miaka 6 wa Aston Villa akionyesha barua aliyoandika kwa Mourinho akimuomba aje kuiokoa timu yake .

Saa 24 zilizopita zimekuwa ngumu sana kwa mashabiki wa klabu ya Aston Villa ambao wameishuhudia timu yao ikianguka kwenye janga la kushuka daraja baada ya mfululizo wa matokeo mabaya.

Kama hiyo haitoshi timu hiyo pia imemfukuza kocha wake na kwa muda wa siku nzima imekuwa ikihaha kuajiri kocha mpya ambaye ataiongoza klabu hiyo kwenye mchezo wake unaofuata wa ligi kuu ya England.

Katika hali isiyo ya kawaida na ya kuhuzunisha shabiki mmoja wa klabu hiyo Jude Branson amemuandikia kocha wa ChelseaJose Mourinho barua isiyo rasmi akimuomba ajitolee na kuisaidia timu hiyo siku chache kabla  ya kufukuzwa kwa kocha Paul Lambert.

Shabiki mwenye umri wa miaka 6 wa Aston Villa akionyesha barua aliyoandika kwa Mourinho akimuomba aje kuiokoa timu yake .

Shabiki mwenye umri wa miaka 6 wa Aston Villa akionyesha barua aliyoandika kwa Mourinho akimuomba aje kuiokoa timu hiyo.

Kijana huyo aliandika barua fupi ambayo ilikwenda moja moja kwenye lengo ambapo ilikuwa imeandikwa hivi; “Kwako Mr Mourinho, jina langu ni Jude nina umri wa miaka sita na ni shabiki mkubwa wa Aston Villa, wewe ndiye kocha bora kwa upande wangu, tafadhali unaweza kuifundisha timu yetu na pia uje na mshambuliaji wako Diego Costa? tunahitaji msaada, asante sana, mimi ni Jude Branson“, akaishia hapo.

Mourinho

Kwa bahati mbaya Mourinho hakuweza kutimiza ndoto za shabiki huyu kwani ana mkataba wa kuifundisha Chelsea na kwa jinsi timu hiyo inavyofanya kwenye ligi kuu ya England kwa sasa ni vigumu kudhani kuwa bilionea Mrusi, Roman Abramovich anaweza kukubali kuona Mreno huyu akiondoka na kuiacha klabu yake kwenye mataa.

Mourinho hata hivyo alimjibu Jude Branson kwa kumtumia picha yake mwenyewe ambayo ameiwekea sahihi yake kama ukumbusho.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments