Top Stories

Atakayofanya Rais Samia akiwa Rwanda

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Agosti 2, 2021 anatarajia kuanza ziara ya Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili nchini Rwanda kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo  Paul Kagame.

Akiwa nchini humo, Rais Samia pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame, kisha atashuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari.

Ziara hiyo ya siku mbili inalenga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano baina ya Rwanda na Tanzania.

RAIS AAGIZA WATAKAOCHOMWA CHANJO WALIPWE DOLA 100, WENGINE KUPIMWA

Soma na hizi

Tupia Comments