Katika kutanua wigo wa safari zake za kimataifa, Kampuniya Ndege Tanzania (ATCL) iko kwenye maandalizi yakuanzisha safari za moja kwa moja kuelekea Muscat nchini Oman.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi alisema haya baada yakukutana na Balozi wa Oman nchini Mhe. Saud bin HilalAlshaidani tarehe 26 Juni 2024 katika Ofisi za Ubalozizilizopo jijini Dar es Salaam.
“Taratibu za kufungua kituo nchini Oman zimeanzaambapo Air Tanzania tumeshampata wakala mkuu wamauzo ya tiketi zake nchini Oman (General Sales Agent), tumeteua Msimamizi wa Kituo hicho” alisema MhandisiMatindi na kuongeza kuwa kwa sasa hatua iliyofikiwa nikukamilisha uandaaji wa timu ya marubani, ndegeitakayotumika pamoja mpangilio wa safari.
Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saud bin HilalAlshaidani alisema mazungumzo yake na Air Tanzania yamekuwa na tija ambapo wamejadili fursa zilizopo kwakutumia ndege za abiria na mizigo.
“Kwa idadi kubwa ya raia wa Oman waliopo hapa nchini,biashara kati ya nchi hizi mbili ikiendelea kukuzwa, nimatarajio yangu kuwa Air Tanzania itanufaika na fursa hiipasi na mshindani bali mshirika kwa upande wa abiria namizigo“, alisema Mhe. Balozi Alshaidani na kutaja mazaomatatu yanayoweza kuwekewa msisitizo.
“Tunaweza kujikita kwenye usafirishaji wa aina tatu tu zamatunda zenye uhitaji mkubwa nchini Oman, maembe, nanasi na parachichi. Hii itanufaisha pande zote, wafanyabiashara wa Tanzania na Oman”.
Kwa sasa Air Tanzania inafanya safari za ndani na nje yanchi. Kwa safari za kikanda na kimataifa ina safari zaDubai (UAE), Mumbai (India), Guangzhou (China), Bujumbura (Burundi), Entebbe (Uganda), Hahaya(Comoro), Harare (Zimbabwe), Lusaka na Ndola(Zambia), Nairobi (Kenya) na Lubumbashi (Congo). Kwa Tanzania ATCL imekuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es salaam kwenda mikoa ya Dodoma, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Songea, Katavi, Zanzibar, Mtwara, Tabora na Kigoma.
Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Saud bin HilalAlshaidani (kulia) akimueleza Mkurugenzi Mtendaji waKampuni ya Ndege Tanzania Mha. Ladislaus Matindinamna wanavyoweza kushirikiana kibiashara kwa nchihizo mbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege TanzaniaMha. Ladislaus Matindi akimkabidhi Jarida la Twigalinalotumika ndani ya ndege hizo Balozi wa Oman nchiniTanzania Mhe. Saud bin Hilal Alshaidani (kulia) baada yamazungumzo kuhusu kukuanzisha safari za Oman.