Habari za Mastaa

‘Nina mpango siku yoyote kuzivunja tuzo za KTMA nilizoshinda’ – AT

By

on

Msanii wa muziki wa Miduara kutoka Zanzibar Ally Ramadhani aka ‘AT’ amesema ana mpango wa kuzivunja tuzo zote alizowahi kushinda kupitia Category mbalimbali kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) sababu amesema kuwa haoni faida ya tuzo hizo kwa sasa.

AT amezungumza kwenye XXL ya Clouds FM kwa kusema>> ‘Yaani nina mpango siku yoyote zile tuzo za KTMA nazivunja,sitakaa na tuzo hata moja sizitaki sababu kila nikizona na matukio ambayo yapo najisikia vibaya sana sababu naamini ningekua nimepiga hatua’

Sentensi zingine alizosema AT >> ‘Sababu ni watu ambao wanasema mtu yoyote akija tutamsaidia lakini mimi nimekwanda pale pamoja na kuwa nilikua na ahadi walishindwa kunisaidia,nikaona wananidharau haina haja ya kubaki na  makopo, siku nitakayovunja nitaweka Instagram, Hawawezi kunishtaki zile tuzo ni za kwangu’ -AT

Unajua kama AT na Dayna Nyange hawakumchagua Rais Magufuli? Wameyazungumza haya kwenye uongozi wake.

Tupia Comments