Michezo

Atletico vs Barca nani bingwa La Liga: Tazama video za mechi zao jana

on

BnYEwWRCEAA52hK.jpg-mediumBingwa wa ligi kuu ya Hispania ataamuliwa kwenye mchezo baina ya FC Barcelona dhidi ya Atletico wikiendi ijayo.

Atletico, hawajafungwa kwenye mechi tano dhidi ya Barca msimu wa 2013-14, sasa wanahitaji pointi moja tu ili waweze kuchukua ubingwa jumapili ijayo kwenye dimba la Camp Nou, wakati FC Barcelona watahitaji ushindi kwenye mechi hiyo ili wafikishe pointi 89 na kuweza kuchukua ubingwa wa rekodi nzuri dhidi ya Atletico. ( head-to-head record.)

Ushindi kwa Barca utamaanisha Barca watakuwa na pointi sawa na Madrid wenye pointi 89, lakini Barca wataweza kutawazwa kuwa mabingwa kutokana na kuwa na rekodi nzuri dhidi ya Atletico kwenye La Liga – mechi ya kwanza walitoka sare 0-0 na endapo watashinda jumapili watakuwa na rekodi bora dhid ya Atletico kwenye head to head.

FC BARCELONA VS ELCHE

Highlights Elche CF (0 -0) FC Barcelona La Liga… by elencrist001

ATLETICO MADRID VS MALAGA

Atletico Madrid 1-1 Malaga (11-05-2014… by linhmu275

Tupia Comments