Mix

Watoto wa Mwalimu Nyerere wapigana vikumbo ubunge Butiama

on

Wanafamilia watatu wa familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge Jimbo la Butiama mkoani Mara, Wanafamilia hao ni Makongoro Nyerere na Madaraka Nyerere ambao ni mtu na mdogo wake na watatu ni Jacton ambaye ni mtoto wa kaka wa Mwalimu Nyerere.

Akizungumzia tukio hilo ambalo si la kawaida sana, Katibu wa CCM Wilaya ya Butiama, Moza Abdallah amesema ndugu hao wametumia haki yao ya kikatiba ya kugombea ndani ya chama.

Ameongeza kuwa pamoja na wanafamilia hao kiwa miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu kuomba ridhaa ya chama hicho, lakini ukweli ni kwamba anatakiwa mtu mmoja pekee ambae atasimama katika jimbo hilo kwa ajili ya kukiwakilisha chama kwenye uchaguzi mkuu baada ya taratibu zote kufuatwa.

CHANZO: TBC

Soma na hizi

Tupia Comments