Ishu ya shambulio lililotokea kwenye Chuo Kikuu cha Garissa Kenya bado imeendelea kuchukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari duniani.
Kikubwa kilichosikika leo April 6 2015 ni kuhusu watu mbalimbali kuendelea kujitokea ili kutambua miili ya ndugu zao waliouawa katika shambulio hilo la kigaidi, zoezi hilo limeendelea kwa siku ya nne katika Hospitali ya Chiromo.
Miili ya watu 126 tayari imeshatambulika, mpaka sasa miili ambayo haijatambulika ni ya watu 20.
Baadhi ya ndugu bado hawajatambua miili ya ndugu zao kitu ambacho kinawatia wasiwasi huku wengine wakikataa kurudi tena kutafuta miili ya watoto wao kutokana na miili hiyo kuwa imeharibika.
“Mimi mwenyewe nimeingia kwa ile mochuari Friday niliingia na Jumamosi tuliingia zile mwili ziko hata uonyeshwe huyu ni mtu wako huwezi tambua zimeharibika kabisa.. hapa nimepitia miili 50, nyingi zimeharibika hata ukiangalia sana akili inachanganyikiwa hata leo sizani kama naweza kuingia nangojea tuu watuite…” aliongea mzazi mmoja aliyekuwa nje ya .
Serikali ya Kenya imeendelea na jitihada za kuwasaidia watu kutambua miili ya ndugu zao kwa kutumia mashine maalum inayosoma alama za vidole.
Ili kusikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24 bonyeza play hapa chini…
Kaa karibu na millardayo.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook