Ikiwa ni miezi miwili tangu kutokea kwa shambulio la wanamgambo wa kiislamu katika mji wa Bardo, Tunisia, headlines zimerudi tena nchini humo baada ya shambulio lingine kutokea saa chache zilizopita katika moja ya hoteli za kitalii pwani ya Tunisia na kusababisha vifo vya watu 27.
Maafisa wa Serikali ya Tunisia wamesema tayari mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa ulinzi huku wengine wakiendelea kusakwa.
Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Sousse, sehemu ambayo ni maarufu na watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani hupendelea kutembelea.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi hiyo amesema kuna watu wengine sita wamejeruhiwa katika shambulio hilo na jeshi la ulinzi linaendelea kuwatafuta wahusika.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.