Mix

Safari ya Obama kwenda Kenya iko palepale.. Safari ya Miss World je?

on

Rolene Strauss

Hali ya nchi ikiwa sio nzuri kuna vingi vinaathirika, unaweza ukaona kwa haraka haraka tu kwamba athari kubwa ni vifo na uharibifu wa mali za watu.. lakini ukiiangalia kiundani athari yake ni kubbwa zaidi ya hapo.

Rolene Strauss ni mrembo wa South Africa ambaye alifanikiwa kushinda taji la Miss World 2014, leo ndio nimejua kwamba mrembo huyu alikuwa na ratiba ziara yake Nairobi Kenya na ilikuwa afanye hafls ya chakula cha usiku Nairobi March 10 2015 !!

Kutokana na ishu ya mashambulizi ambayo yametokea Chuo Kikuu cha Garissa Kenya, Rolene ameahirisha safari yake na amesema yeye pamoja na timu ya watu wake ilikuwa aje nao Kenya watatangaza tarehe nyingine ya kuja kwa ajili ya kuja Kenya.

Obama II

Kama hukujua ni kwamba mashambulizi ya Chuo hicho yamefanyika muda mfupi baada ya Rais Obama kutangaza kuwa atatembelea nchi hiyo July 2015.. hata baada ya mashambulizi kutokea bado amesema ratiba yake iko palepale.

Kaa karibu na mtu wako wa nguvu kwenye millardayo.com, nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa>>>twitterInsta Facebook

Tupia Comments