Mwili wa mwanaume ambaye Jina lake halijafahamika umekutwa umeuwawa vichakani ukiwa na jeraha usoni huku ikioneshwa kunyweshwa simenti.
Mwili wa mtu huyo umeonekan katika vichaka vya mlima wa Uledi kata ya mpela manispaa ya Tabora Novemba 16,2024 baada ya waponda kokoto wa eneo hilo kubaini kuwa Kuna mwili katika eneo hilo.
Mashuhuda wa tukio hilo Enock Msonde na Pili Issa wanaojishughulisha na uchimbaji wa mawe na kuponda kokoto wamesema mwili huo wameukuta ukiwa na saruji mdomoni na puani na kupata hisia kuwa mtu huyo aliuawa kwa kupigwa na kunyweshwa saruji.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Richard Abwao amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na amesema uchunguzi wa kubaini chanzo cha tukio hilo unaendelea utakapokamilika taarifa itatolewa huku akiwataka wananchi au ndugu kufika katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora – Kitete kwa ajili ya kutambua mwili huo.