Top Stories

Auawa kwa kusababisha timu yake kufungwa

on

Kutokea nchini Uganda Churchill Owaci (22) ameuawa na wachezaji wenzake kwa kufanya makosa yaliyopelekea kufungwa goli katika mechi ya kirafiki baina ya timu mbili za mtaani.

Mwenyekiti wa Kaunti Ndogo ya Agoro, Denis Onyon amesema, wachezaji wenzake walimpiga na baada ya mchezo Owaci alitaka kulipa kisasi kwa kumvuta mchezaji mwenzake kwenye baiskeli hali iliysababisha ugomvi zaidi.

Msemaji wa Polisi, ASP Jimmy Patrick Okema amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema wanawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea.

KILICHOSABABISHA MOTO MLIMA KILIMANJARO “WANAPASHA CHAKULA UKASHIKA NYASI”

Soma na hizi

Tupia Comments