Top Stories

Auawa na mdogo wake akimzuia kulala na shemeji yake (+video)

on

Jeshi la Polisi Arusha linamshikilia Melita Ndaletyani wa Noondoto Wilayani Longido kwa tuhuma za kumuua Kaka yake aitwae Kiseri Ndaletyani kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni.

Melita anadaiwa kufanya hivyo kwenye ugomvi uliotokana na Kaka huyo kumzuia kutaka kufanya mapenzi kwa lazima na Shemeji yake ambae ni Mke wa Kiseri.

Kamanda wa Polisi Arusha Justine Masejo amesema kifo cha kaka yake kilitokana na ugomvi uliotokea wakati akimzuia Mdogo wake kulazimisha kulala kimapenzi na Shemeji yake “Usiku wa kuamkia leo saa sita na nusu usiku Kiseri (38) ambae ni Mfugaji alifariki baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali”

“Mdogo wake Melita (34) alitaka kumuingilia kinguvu Mke wa Kaka yake, sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na upelelezi ukikamilika jalada litafikishwa ofisi ya mashtaka kwa hatua za kisheria” ——— RPC Masejo.

Soma na hizi

Tupia Comments