Michezo

AUDIO: Antonio Nugaz aweka wazi suala la Lamine Moro, Dante kapotezewa?

on

Afisa muhamasishaji wa mkuu wa Yanga SC Antonio Nugaz ameamua kueleza na kuweka wazi kuwa wamemlipa madeni yake beki wao Lamine Moro aliyekuwa amegoma, lakini wengi wakahoji mbona Lamine kagoma muda mfupi kalipwa lakini Andrew Vincente ‘Dante’ hajalipwa hadi leo hii.

“Kuhusu suala la Lamine Moro alikuja na mapendekezo yake ya kuvunja mkataba kwa hiyo katika kuvunja mkataba ule akaiwasilisha barua changamoto za hapa na pale, kwa hiyo uongozi haukumjibu kwamba ndio kama hujajibiwa na mshahara umeingiziwa wewe unabaki kuwa mali ya club”>>>Nugaz

“Kwani Lamine Moro alikuwa anadaiwa kama anavyodai Dante? Dante kaenda yeye kutushitaki Lamine Moro hajashitaki alikwenda kuomba kuvunja mkataba, hata Dante kesi yake ipo inashughulikiwa na mshahara inaingizwa kama kawaida nadhani kila kitu kipo sawa” >>>Nugaz

VIDEO:PAMBANO LA ROUND 10: MWAKINYO VS TINAMPAY

Soma na hizi

Tupia Comments