AyoTV

AUDIO: Kuelekea Pambano la Ubingwa wa Dunia kati ya Mtango vs Tatakhun

on

Bondia Mtanzania Salim Mtango ametamba kubakisha ubingwa wa dunia wa UBO nchini Tanzania mara atakapocheza pambano lake la Ubingwa wa Dunia January 31 2020 jijini Tanga dhidi ya Suriya Tatakhun wa Thailand katika pambano la round 12.

Pambano hilo lililoandaliwa na promota  Ally Mwanzoa litapigwa January 31 kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku likitanguliwa na mapambano mengine 6 ya utangulizi moja kati yao likiwa la Ubingwa pia.

Mtango kwa sasa yuko kambini jijini Dar es Salaam chini ya kocha Rashid Matumla ambaye anamnoa kuhakikisha anafanya maandalizi yatakayomfanya kuwa Bingwa, promota wa pambanoAlly Mwanzoa amesema maandalizi yamekamilika na mpinzani wa Mtango atawasili nchini siku saba kabla ya pambano.

VIDEO: KINACHOENDELEA VILLA PARK SASA HIVI, SAMATTA AKISUBIRIWA KUTANGAZWA

Soma na hizi

Tupia Comments