Hivi karibuni serikali ya Tanzania ilitangaza kuzuia ndege za abiria kutua Tanzania kwa sababu ya kuepuka maambukizi ya virusi vya corona huku ikiruhusu ndege za mizigo pekee kuingia nchini lakini zingine zikiwekewa vizuizi pia.
Azam FC ni miongoni mwa club za Tanzania ambazo zina wachezaji wengi wa kigeni lakini pia asilimia 99 ya benchi lake la ufundi ni raia wa kigeni na kwa sasa wachezaji wao wa kigeni na makocha wao wapo katika mataifa yao,
vipi inakuwaje kama serikali ikiruhusu mechi za VPL kuendelea kuchezwa bila mashabiki ili kumalizia msimu, Azam FC watafanyaje kuwapata wachezaji wao na makocha wa kigeni wakati ndege zimezuiwa kuingia nchini? Afisa habari wa Azam FC Thabiti Zacharia ameongea na AyoTV.
VIDEO: SAMATTA AELEZEA HALI YA LOCKDOWN INAVYOMTESA ENGLAND