Top Stories

Awalisha abiria dawa za kikongo

on

Jeshi la Polisi Mkoani Mara linamshikilia Marco Abdul (68) mkazi wa kijiji cha Rugasha Katoro mkoani Kagera kwa tuhuma za kuwalisha abiria ndani ya mabasi dawa za kienyeji zinazojulikana kwa jina la ‘khabharagata’ zinazoagizwa kutoka Congo kwa lengo la kuwalewesha abiria na kisha kuwaibia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 7, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibushubwamu amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kituo cha mabasi wilayani Bunda mkoani Mara baada ya kumywesha abiria mmoja.

Amesema mtu huyo akishirikiana na watu wengine watano (bado hawajakamtwa) wamekuwa wakiwanywesha abiria dawa hizo kwa kuziweka kwenye maji au soda na kupaka kwenye biskuti au pipi kisha kuwapa abiria ambao baada ya kunywa hujikuta wamelewa na kupoteza fahamu.

EXCLUSIVE: FUNDI ALIYENUSURIKA KIFO GOROFA LA GOBA ASIMULIA “LILISHUKA GHAFLA WAAAH, NIKARUSHWA”

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments