Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amehakikisha Kazi iliotakiwa kufanyika ndani ya wiki moja ya ukamilishaji wa Mradi wa Maji wa Buhongwa jijini Mwanza ilitokiwa kukamilishwa mpaka ijumaa inafanyika ndani ya siku moja kwa kuamua kuweka kambi na mafundi site mpaka saa tano na nusu usiku.
Mradi wa dharula Buhongwa umekamilika usiku wa saa sita na Maji rasmi yamefika hapa Buhongwa Centre baada ya maunganisho ya bomba na kuwasha mtambo rasmi kusukuma maji.
Awali Waziri Aweso ameshuhidia maunganisho ya bomba ya mwisho ya mradi wa Sahwa Buhongwa ambao unalenga kutatua changamoto katika maeneo ya Sahwa, Lwanhima na Buhongwa.
Mara baada ya bomba la mwisho kuunganishwa saa 4.15 usiku alielekea katika kituo cha kusukuma maji Sahwa ili kuwasha pump ya maji kwa lengo la kusafisha bomba hilo.
Usiku huo huo Waziri Aweso amewakabidhi wenyeviti wa serikali za mitaa za Sahwa chini na Semba mabomba kwa ajili ya kusogeza maji katika maeneo yao.
Jumla ya vituo nane vya kuchota maji vitajengwa katika maeneo hayo na kunufaisha wananchi katika mitaa husika.