Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Kylie Jenner kutumia zaidi ya Bilioni 2 kwenye birthday yake (+picha)

on

Baada ya mfanyabiashara maarufu nchini Marekani Kylie Jenner kutajwa na jarida la Forbes kuwa ana utajiri wa dola Bilioni 1 za Kimarekani inaelezwa kuwa pesa sio kitu kwake kutokana na kuripotiwa kufanya sherehe yenye gharama kubwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa ifikapo August 10 mwaka huu basi Kylie Jenner ana mpango wa kukodisha boti ya kifahari (Yatch) kwa ajili ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa ambapo atatimiza miaka 22. Inaelezwa kuwa kukodisha yatch hiyo iitwayo Tranquility kwa wiki itagharimu dola za Kimarekani Mil 1.2 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 2 za Kitanzania.

Inaripotiwa kuwa yatch hiyo ina uwezo wa kubeba watu 22 , vyumba 10 binafsi , saluni, sehemu kwa ajili ya kuangalia filamu (theatre), bwawa la kuogolea (swimming pool).

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA NANDY KATOA YA MOYONI KWA MSANII ANAYEMSEMA VIBAYA “ANAWIVU HATUENDANI”

Soma na hizi

Tupia Comments