Habari za Mastaa

Album ya ‘Father of Asahd’ yafikisha mauzo ya nakala zaidi ya laki 5 ndani ya mwezi

on

Inaelezwa kuwa Album ya mtayarishaji maarufu duniani wa muziki Dj Khaled “Father of Asahd” imefikia viwango vya mauzo ya gold ambapo mpaka sasa inadaiwa kuwa zimenunuliwa nakala zaidi ya laki 5 toka Album hiyo ilivyoachiwa rasmi May 17,2018.

Album hiyo yenye jumla ya ngoma 15 ikiwa imewashirikisha mastaa kibao chama cha Recording Industry Association of America (RIAA) kimemkabithi cheti Dj Khaled. Kutokana na mafanikio hayo Dj Khaled ameahidi kutoa surprise kibao endapo Album hiyo itafikia mauzo ya nakala zaidi ya Million 1 (Platnum) na ameyasema hayo kupitia ukuarasa wake wa instagram.

Siku kadhaa zilizopita Dj Khaled alionekana kukerwa kutokana na Album ya ‘Father of Asahd’ kushindwa kushika nafasi ya kwanza katika chart za Billboard na kuelezwa  kuwa alizua balaa kwa waandaji wa chart hizo kubwa duniani.

VIDEO: ULIPITWA NA SIKU 7 ZA WEMA GEREZANI ZAMTESA AUNT EZEKIEL? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA 

Soma na hizi

Tupia Comments