Mawakala wa kupeleka Wanafunzi kusoma nje ya Nchi Global Education Link kupitia kwa Mkurugenzi wake leo May 31, 2017 wamekutana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo amejibu maswali yaliyohusu Kozi ya udaktari nchini.
Baada ya mkutano huo Madaktari wa Muhimbili wameuelezea mkutano huo wakisema wao kama Taasisi wana lengo la kupeleka watu kwa ajili kusoma masomo ya muda mfupi:>>>“Leo tumekutana na watu wa Globa Education Link ambapo tulikuwa na mkutano na Madaktari wote pamoja na Wauguzi.
“Tunachojaribu ni kutafuta Link sisi kama Taasisi na Vyuo vya Nje ili kuweza kupeleka watu kwa ajili ya course za muda mfupi ambazo Taasisi itaweza kuchangia yenyewe.” Prof. Mohamed Janabi (Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo)
Ulimiss hii Good News! Waliomaliza Form Six na Diploma wanaotaka kusoma Nje Ya Nchi. Itazame hii video hapa chini.