Habari za Mastaa

VIDEOFupi: Pilau la harusi linanukia? AY kafuata alichokifanya Profesa Jay

on

Speed ya mastaa wa Bongofleva kuamua kuweka wazi mahusiano yao ya kimapenzi inazidi kuwa kubwa, leo kwenye headlines ni hodari mwingine wa Bongofleva mkali wa hit singles za kutosha AY ambaye amekuwa akionekana kuzama kwenye huba na mrembo Remy kutoka Rwanda, sasa kingine kikubwa amekifanya staa huyo ni hiki cha kumvisha pete ya uchumba.

AY anakuwa moja kati ya mastaa ambao huenda wakaingia kwenye ndoa hivi karibuni na hili linathibitishwa na video iliyowekwa na mpiga picha maarufu Mx Carter ambayo imemuonesha AY akiwa kwenye eneo ambalo halikufahamika alipiga magoti na kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo raia wa Rwanda.

Nimekuwekea hapa chini kipande cha video, kitazame.

VIDEO: Zipo hapa dakika 18 za AY, Sugu, Black Rhyno wakiwa kwenye harusi ya mkongwe Profesa Jay. Bonyeza play kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments