Habari za Mastaa

Nikki wa Pili kuhusu kauli ya JPM ‘Hakuna mwenye mimba atakayerudi shuleni’

on

Siku moja baada ya Rais JPM kusema katika utawala wake hakutakuwa na mwanafunzi mwenye mimba atakayerudi shule baada ya kujifungua, kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na watu mbalimbali mmoja wao akiwa staa wa Bongofleva Nikki wa Pili.

Nikki wa Pili aliandika kwenye Twitter yake:>>>”Ukimpa mwanfunz mimba jela miaka 30 mama anafukuzwa shule baba yuko jela mtoto huyu nae itakuwa ngumu pia kuepuka mimba ya utotoni #mzunguko, Mimba ndio njia yetu ya kuja duniani na mwanamke ndio shujaa wetu daima nampa nyota begani.” – Nikki wa Pili.

Baada ya tweet hiyo Ayo TV na millardayo.com zimempata Nikki wa Pilli ambaye anafafanua zaidi kuhusu kauli ya Rais Magufuli na alichokiandika kwenye Twitter.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full Story

“Hakuna mwenye mimba atakayerudi shuleni” – Rais Magufuli.

Maamuzi ya Dogo Janja baada ya Jux kupata Degree, China (+Video)

Soma na hizi

Tupia Comments