Michezo

Azam FC imeipa Yanga SC baraka za kumsajili Ditram Nchimbi

on

Club ya Azam FC imethibitisha kuwa imelipwa fidia na Yanga SC kwa ajili ya kumuachia mshambuliji wao Ditram Nchimbi aliyekuwa kwa mkopo Polisi Tanzania ajiunga na Yanga SC, Nchimbi alikuwa kabakiza mkataba wa miezi 6 na Azam FC.

Afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga ndio amethibitisha taarifa hizo kupitia kipindi cha Mshikemshike cha Azam TV kuwa wamemruhusu Nchimbi baada ya mchezaji huyo kuonesha nia ya dhati ya kujiunga na Yanga.

“Club ya Yanga ilionesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo (Nchimbi) kwa ajili ya dirisha dogo, jana Yanga wameleta barua lakini tumeongea na mchezaji mwenyewe ameonesha nia ya dhati ya kwenda kwenye club ya Yanga, Yanga wameshalipa kile ambacho sisi tunakihitaji” >>>> Jafari Iddi Mganga

Soma na hizi

Tupia Comments