Baada ya mvutano wa mgogoro wa Kimkataba wa muda mrefu kati ya Yanga SC na Feisal Salum hatimae leo suala hilo limefikia tamati.
Yanga SC wametoa taarifa ya kuwa wamepokea ofa kutoka Azam FC na kuamua kumuuza mchezaji huyo kwenda Azam FC baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Feisal anaenda Azam FC kwa ada ya uhamisho ambayo ni siri, ikumbukwe kuwa Feisal yuko nje ya uwanja toka 24/12/2022 alipoandika barua ya kuomba kuvunja mkataba na Yanga.
Saa chache baada ya taarifa hiyo kutoka Azam FC wamemsainisha Feisal Salum mkataba wa miaka mitatu na atakuwa Chamazi hadi 2026, Feisal amepewa jezi namba 6 baada ya utambulisho huo.