Michezo

Azam FC watinga robo fainali ya Kombe la FA

on

Club ya Azam FC hatimae imetinga robo fainali ya michuano ya Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup) kwa kuifunga Polisi Tanzania 2-1.

Magoli ya Azam FC yalifungwa na Mzimbabwe Prince Dube dakika ya 25 na 65 kwa mkwaju wa penati na baadae Polisi Tanzania kupitia Marcelo Kaheza akafunga goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati dakika ya 76.

Timu za Azam FC na Biashara United ndio wanatinga robo fainali huku wakisubiri kujua wataungana na timu gani nyingine sita kutimiza nane bora (robo fainali), kesho ni Mwadui FC vs Coastal Union na Prisons vs Yanga.

Soma na hizi

Tupia Comments