Club ya Azam FC ambayo mmilili wake Yusuph Bakhressa alinukuliwa akisema unyonge sasa basi mashabiki wake wafurahie na atafanya usajili mkubwa na wenye tija kwa club leo ametangaza kusajili Mikel Guillen Raia wa Hispania kama kocha wa utimamu wa mwili (fitness coach).
“Tunayo furaha kumtambulisha, Mikel Guillen, kutoka Hispania kama Kocha mpya wa viungo wa klabu yetu, Guillen ni kocha wa viwango vya juu, mwenye uzoefu wa kufundisha timu za Aris Limassol ya Cyprus, inayoshiriki Ligi ya Conference European Cup, Bengaluru ya India na Dinamo Bucuresti ya Romania”
“Uzoefu wake umemfanya kufundisha baadhi ya wachezaji wakubwa, akiwemo Sunil Chhetri, mfungaji namba sita wa mabao duniani kwa upande wa timu za Taifa, Wengine aliowanoa ni Gordon Schildenfeld, aliyecheza fainali za Kombe la Dunia na Euro akiwa na Taifa lake la Croatia na Manu Garcia, aliyewahi kuwa nahodha wa Alaves kwa zaidi ya mechi 100 kwenye La Liga”
Club ya Azam FC hadi sasa imetambulisha wachezaji Cleophace Mkandala, Nathaniel Chilambo, Abdul Eleman Sopu, Isah Ndala kutokea Nigeria, Tape Edinho kutokea Ivory Coast, Kipre Junior kutokea Ivory Coast pamoja na kocha wa magolikipa Dani Cadena kutokea Hispania na Kali Ongala kocha wa washambuliaji.
MZEE MPILI KWENYE MKUTANO WA YANGA “MIMI NIKO UPANDE WA TAKUKURU NITAWACHUKULIENI HATUA 😂😂”