Michezo

Azam FC yamsajili Khleffin aliyekuwa kivutio cha kocha wao Cioaba

on

Club ya Azam FC inayofuraha kuwataarifu kuwa tumekamilisha taratibu za kumsajili kiungo mshambuliaji  Khleffin Hamdoun kutokea Mlandege FC ya Zanzibar kwa mkataba wa miaka minne.

Huo unakuwa usajili wa kwanza kwa Azam FC kwenye dirisha dogo la usajili, likiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, Hamdoun aliyefikisha umri wa miaka 19 leo, amesaini mkataba rasmi wa kuitumikia Azam FC leo Jumatano usiku, mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Mara baada ya kusaini mkataba huo, kiungo mshambuliaji huyo alielezea furaha yake ya kukamilisha taratibu ya kujiunga Azam FC huku akiahidi kushirikiana na wachezaji wenzake kuipa mataji timu hiyo, Kiungo mshambuliaji huyo alionyesha kiwango kizuri akiwa na timu yake ya Mlandege ilipochuana na Azam FC juzi katika mchezo wa Mapinduzi Cup 2020, jambo ambalo lilimvutia Cioaba na kuidhinisha asajiliwe haraka iwezekanavyo.

Soma na hizi

Tupia Comments