Michezo

Rekodi mpya ya Azam FC na matokeo yao vs Tanzania Prisons haya hapa

on

IMG_2655Mabingwa watetezi wa Tanzania bara Azam FC leo imeweka rekodi mpya katika Vodacom Premier League baada ya kukamilisha idadi ya mechi 37 za ligi hiyo bila kupoteza hata mchezo mmoja.

Azam FC leo hii walikuwa ugenini kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya walikuwa wakipambana na ‘Wajela Jela’ Tanzania Prisons.

Matokeo ya mchezo huo ni sare ya bila kufungana.

Azam FC msimu uliopita iliifikia rekodi ya Simba ya kumaliza ligi na kutwaa ubingwa bila kufungwa, na katika msimu huu mpya imeshinda mechi zake mbili za kwanza kabla ya leo kutoa sare na Prisons.

Matokeo mengine kwenye ligi ni kama ifuatavyo:

Polisi Morogoro 1-1 Kagera Sugar… FT… Coastal Union 2-1 Ndanda FC… FT… Ruvu Shooting 0-0 Mbeya City, Simba 1 – 1 Stand United

Tupia Comments