Michezo

Ushindi huu waipeleka Azam FC Robo fainali Kombe la Kagame 2015

on

Azam_FC11

Klabu ya Azam FC imezidi kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Kagame ambalo linaendelea Dar es Salaam...Azam FC amabayo ilianza kufanya vizuri katika mashindano hayo toka mechi ya kwanza kwa kuifunga KCC ya Uganda kwa goli 1-0, goli pekee ambalo lilifungwa na John Bocco dakika ya 9 ya mchezo.

Kikosi cha azam

July 25 Azam FC imetinga Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezo wake wa mwisho wa kundi C dhidi ya Adama City ya Ethiopia… Azam FC imeifunga Adama City ya Ethiopia kwa jumla ya magoli 5-0 magoli amabyo yamepachikwa wavuni na Kipre Tchetche dakika ya 7 na 19, Farid Mussa dakika 31, Mudathir Yahya dakika ya 49 na Aggrey Morris dakika ya 73 kwa mkwaju wa penati.

f0796-moradi_0-723263

Kwa matokeo hayo Azam FC inaongoza kundi C kwa jumla ya point 9 nyuma ya KCC FC ya Uganda ambayo ipo nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikishikwa na Malakia ya Sudani Kusini na Adama City ya Ethiopia ikishika mkia, sasa  Azam FC itacheza Robo fainali na mshindi wa pili wa kundi A.

DSC02451

 

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie

Tupia Comments