Michezo

Azam FC imemalizana na CEO wake leo

By

on

Ni siku imepita toka Saad Kawemba akanushe kuhusiana na tetesi zake kuwa amefutwa kazi ya afisa utendaji Mkuu wa club ya Azam FC, leo June 1 2017 habari mpya zimeripotiwa kuhusu CEO huyo.

Mtandao wa mchambuzi wa habari za michezo Tanzania shaffihdauda.co.tz umeripoti kuwa rasmi Azam FC wameachana na Saad Kawemba kama afisa mtendaji Mkuu wake baada ya mkataba wake kumalizika.

Azam FC wameachana na Saad Kawemba na kubadili mfumo wa kiutawala, ambapo wamefuta cheo cha CEO na kubaki na cheo General Manager lakini pia wamebadili sera yao ya usajili na kuamua kurudi katika mfumo wa kupandisha vipaji kutoka timu B.

VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera

Soma na hizi

Tupia Comments