Kutoka Bungeni DODOMA, leo April 10, 2017 Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesimama kuomba muongozo kwa Naibu Spika wa Bunge akitaka Bunge lisimamishe shughuli za kawaida na kuanza kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea nchini.
Bashe amesema yeye pia ameshatumiwa ujumbe wa vitisho wakimwambia kuna watu 11 akiwemo yeye watafanyiwa vitendo vibaya popote watakapokuwa, hivyo analiomba Bunge lijadili suala hilo kwa dharula kwasababu sio sawa kukaa kimya.
>>>’Kuna watu wamenitumia jumbe za kuniambia kwamba mimi ni kati ya watu 11 ambao tupo hatarini kufanyiwa vitu vibaya na popote pale nijiangalie ninapokuwa barabarani'<<<
>>>Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana'<<<< –Hussein Bashe
Mbunge Hussein Bashe ameomba mwongozo kuahirishwa kwa Bunge ili kutoa nafasi ya Wabunge wote kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea pic.twitter.com/iktvRqfBtX
— millardayo (@millardayo) April 10, 2017
Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana' >>> Hussein Bashe pic.twitter.com/ngsdWjGftH
— millardayo (@millardayo) April 10, 2017
'Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie'>> Hussein Bashe pic.twitter.com/wCel62l0Vf
— millardayo (@millardayo) April 10, 2017
VIDEO: Umepitwa na hii ya Bashe kuhusu uwekezaji wa Migodi mkubwa kutokuwa na msaada kwenye nchi? Itazame hapa chini