Habari za Mastaa

Baba wa David Ortiz athibitisha Mwanae kuvamiwa na kupigwa risasi (+Video)

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mchezaji wa mpira wa baseball  aliyekuwa akichezea Ligi  ya Marekani David Ortiz’43 anaripotiwa kuvamiwa na kupigwa risasi alipokuwa kwenye moja ya kumbi za starehe nchini Dominican Republic, baba yake mzazi athibitisha taarifa hizo.

Inaripotiwa kuwa David Ortiz alipigwa risasi maeneo ya tumboni siku ya Jumapili June 9,2019 na baadae alikimbizwa hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na kuelezwa kuwa hali yake mpaka sasa haijulikani inaendeleaje,  ripoti nyingine zilidai kuwa Ortiz alipofikishwa hospitalini alisikika akiwaambia madaktari kuwa “Msiniache nife mimi ni mtu mzuri”.

Baba mzazi wa David Ortiz alisema kuwa alipigiwa simu na kupewa taarifa za mwanae kuumia na kukimbizwa hospitalini lakini mpaka sasa hafahamu mwanae amehamishiwa hospitali gani na hali yake ikoje mpaka sasa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa polisi ni kuwa mtuhumiwa tayari ameshakamatwa.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA MWIMBAJI CHRISTIAN BELLA KUMTETEA HAMISA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI

Soma na hizi

Tupia Comments