AyoTV

VIDEO: Kwa ujasiri Kocha wa Simba SC kajitokeza kwa waandishi “Nimehuzunika”

on

Baada ya Simba SC kuondolewa katika michuano ya CAF Champions League dhidi ya UD Songo ya Msumbiji kwa kutoka sare ya 1-1 nyumbani huku ugenini wakiwa wamepata sare 0-0, hivyo wameondolewa kwa kuruhusu goli nyumbani.

Kocha wao Mkuu Patrick Aussems alijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusiana na mchezo, huku akieleza kuwa wamecheza na kuwapa presha UD Songo lakini haijasaidia mwaka jana walikuwa na furaha ila mwaka huu ni huzuni.

“Nimesikitishwa kwa sababu kuwa hii Ligi ya Mabingwa ndio ilikuwa lengo kuu la club, mwaka uliopita tulikuwa na furaha na mwaka huu tuna huzuni lakini niliridhishwa na uchezaji wa timu yangu kipindi cha pili tumecheza na kutengeneza nafasi na kuwapa presha”>>>Aussems

VIDEO: Niyonzima kaeleza kilichotokea kati yake na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments