Michezo

Alvaro Morata rasmi anaondoka Chelsea

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Chelsea ya England Alvaro Morata ameripotiwa kuwa mbioni kujiunga na club ya Atletico Madrid ya nyumbani kwao Hispania kwa mkataba wa mkopo wenye kipengele cha kumnunua mwisho wa msimu.

Morata mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Chelsea mwaka 2017 akitokea Real Madrid ya kwao Hispania hivyo anarejea nyumbani kwao Hispania baada ya kudumu na Chelsea kwa miezi 18, baada ya mkataba wa mkopo kuisha Atletico Madrid wana nafasi ya kumsajili dau la uhamisho wa pound milioni 48.5.

Usajili wa Morata kutoka Real Madrid kwenda Chelsea iliwagharimu Chelsea kulipa pound milioni 60 kama ada ya usajili, Morata ambaye msimu wake wa kwanza England alifunga magoli 15 katika game 23 lakini amekuwa na wakati mgumu kumshawishi kocha Maurizio Sarri amuamini katika nafasi ya ushambuliaji wa kati.

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments