Michezo

Singida United yaipeleka Simba SC jijini Arusha

on

Baada ya bodi ya Ligi kutangaza kuufungia uwanja wa Namfua wa Singida United kwa kupoteza vigezo, club hiyo imetangazaa kuanza kuufanyia mabadiliko uwanja huo.

Singida United iliyo nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara 2019/2020, imeamua kuhamishia michezo yake miwili ya Ligi Kuu katika uwanj wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakisubiri ukarabati wa kiwanja chao kukamilika.

Game dhidi ya Simba SC ilipangwa kuchezwa Jumapili ya October 27 2019 na game dhidi ya JKT Tanzania iliyopangwa kuchezwa October 30 zimehamishiwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid hivyo Simba italazimika kusafiri hadi Arusha.

Soma na hizi

Tupia Comments