Michezo

Baada ya Depay, Man U kukamilisha usajili wa Schneiderlin

on

  Huku tetesi za kuhusishwa na usajili wa beki Sergio Ramos zikizidi kupamba moto, klabu ya Manchester United leo hii wametajwa katika usajili wa kiungo Morgan Schneiderlin kutoka Southampton.

Morgan Schneiderlin ambaye amekuwa akiwindwa na Man United pamoja na Arsenal kwa kipindi cha muda mrefu sasa, anaonekana kuichagua United kuwa klabu yake mpya – huku Arsenal wakijitoa rasmi kwenye harakati za kugombea saini yake.

Kwa mujibu wa gazeti linaloaminika sana nchini Ufaransa – Man United wanategemea kumsaini Schneiderlin kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 25.

 Wakati huo huo mwandishi mkuu wa michezo wa shirika la utangazaji la Uingereza – BBC, Howard Nurse aliandika tweet moja akisema kwamba uhamisho wa Schneiderlin kwenda Man United utakamilika Jumatano.

Pia mpiga picha rasmi wa Manchester United Craig Norwood leo jioni ameanza kumfollow Schneiderlin katika mtandao wa Twitter – jambo lilopelekea mashabiki wengi kuamini uhamisho huo upo karibu.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa, alijiunga na Southampton mnamo mwaka 2008 na akasaidi timu hiyo kurudi ligi kuu mpaka kujitengenezea jina miongoni mwa viungo bora wa kati.

Tupia Comments