Kocha wa zamani wa club ya Arsenal Unai Emery sasa ametangaza rasmi kurejea kufundisha soka nchini Hispania kama kocha mkuu wa club ya Villarreal, baada ya club hiyo leo kumtambulisha rasmi kama kocha wao mkuu toka afutwe kazi na Arsenal.
Unai Emery ,48, anajiunga na Villarreal kama mrithi wa kocha Javi Calleja aliyeoondoka timu hiyo licha ya kumaliza msimu akiiacha Villarreal nafasi ya tano katika msimamo wa LaLiga na kupata nafasi ya kucheza Europa League msimu ujao.
Hii ni mara ya kwanza Unai anarudi kufundisha timu toka alipofukuzwa na Arsenal mwezi November 2019 baada ya kudumu kwa miezi 18 pekee, akiwa kajiunga nao May 2018 kurith nafasi ya Arsene Wenger, Unai amewahi kufundisha kwa mafanikio vilabu vya PSG, Sevilla na Valencia.
VIDEO: KIMENUKA YANGA, MORISSON KASUSA AKIMBIA NJE UWANJANI “ACHA MASHABIKI WANIPIGE”