Top Stories

“Baada ya kumuua Soleimani, dunia ni salama kwa sasa” – Pompeo

on

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kwa sasa Dunia ni sehemu salama baada ya kifo cha Jenerali wa Iran, Qasem Soleimani aliyeuwawa kwa shambulio la Marekani lililofanyika kwa ruhusa ya Rais Donald Trump, moja ya mabadiliko yaliyoshuhudiwa baada ya shambulio hilo ni pamoja na bei ya mafuta duniani kupanda kwa 4%.

“Alikua Mtu hatari, alikua akipanga mashambulizi dhidi ya Marekani, tusingeweza kuvumilia Mtu yeyote mwenye mipango ya kuwaumiza au kupoteza maisha ya Wamarekani, Rais Trump amefanya maamuzi sahihi”

“Mipango ya Soleimani kufanya mashambulizi ya kigaidi kwa Marekani ilikua ni hatari zaidi kuliko hatua tulizozichukua wiki iliyopita za kumuua” – Pompeo.

Soleimani alikuwa Mtu muhimu kwenye mapambano ya kimkakati mashariki ya kati kupitia vikosi vya kikurdi ambavyo vinafanya oparesheni kwa ushirikiano na Jeshi la ulinzi la Iran, unaambiwa alianza kupata umaarufu alipopewa nafasi ya kuongoza kikosi cha Quds na kujenga ushirikiano wa karibu na kiongozi Mkuu wa kidini Ayatollah Khamenei.

Meja Jenerali Qasem Soleimani na vikosi vyake walikua wakifanya kazi chini ya Kiongozi mkuu wa kidini aitwae Ayatollah Ali Khamanei na sio kufata muundo wa kawaida wa kijeshi wa Iran.

MTANZANIA ALIEKATIKA MGUU SOMALIA KWENYE SHAMBULIO LA AL-SHABAAB

MTANZANIA ANAELIPWA KWA KUCHOMA MAITI ZA WACHINA

Soma na hizi

Tupia Comments