Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Nyakoro Sirro amewavalisha cheo na kuwaapisha SACP Camilius Mwongoso Wambura na ACP Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi, baada ya kupandishwa cheo hicho na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan.
Kamishna wa Polisi (CP) Wambura ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) na Kamishna wa Polisi (CP) Hamad amekuwa Kamishna wa Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi.
Baada ya kula viapo vyao vya utii, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IJP) Sirro amewataka Makamishna hao kufanya kazi kwa bidii na weledi katika nafasi hizo mpya na kwenda kuondoa changamoto katika kamisheni hizo.